YANGA YAJIONDOA KAGAME

Uongozi wa klabu ya Yanga umekataa mualiko wa kushiriki michuano ya kombe la Kagame inayofanyika mwezi ujao nchini Rwanda


Kulingana na taarifa iliyotolewa na Yanga mapema leo, uongozi wa timu hiyo umesema idadi kubwa ya wachezaji wake wamemaliza mikataba


Aidha, taarifa hiyo imesema wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo baadhi bado hawajakamilisha taratibu za usajili huku wengine wakiwa wanakabiliwa na michuano ya Afcon


Pia taarifa hiyo imeongeza kuwa wachezaji wengine wenye mikataba wameruhusiwa kwenda likizo


Yanga ilialikwa kushiriki michuano hiyo mwaka huu ikiungana na Simba na Azam fc kutoka Tanzania


Simba pia imejitoa, Azam Fc mabingwa watetezi wamethibitisha watashiriki


Comments