Kwa wale mnaotumia sana usafiri wa umma au daladala utakuwa umekumbana na mojawapo ya ya vituko vya makonda na abiria wa daladala kama ifuatavyo
- Mlokole; konda weka nyimbo za Yesu
- Konda; Yesu bado hajatoa albam.
- Matozi; humu ndani joto
- Konda; kapande friji
- Abiria; kuna siti?
- Konda; Kwani hawa walioko wamekalia madumu?
- Sistaduu: Konda unanibana
- Konda; hiyo suruali inakubana mbona husemi!
- Mama: sikai siti za mwisho
- Konda; Kwani hizo siti za mwisho ziko nje ya gari?
- Abiria : we konda vipi kuwa kama umeenda shule
- Konda: Mimi ndiyo kwanza nimetoka shule
Kama una mengine tafadhali ututumie na tutakuwekea kiunganishi cha blogu au web yako hapa bure.
source:mpekuzi
Comments
Post a Comment