Tetesi za usajili wa wachezaji barani Ulaya


Romelo LukakuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe, Lukaku atafanikiwa kutua Inter Milan

Inter Milan wanaendelea kupiga hesabu za kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku lakini klabu yake Manchester United imemthaminisha kwa Pauni milioni 62, sawa na Euro milioni 70. (Sportmediaset - in Italian)
Uhamisho huo wa Lukaku, 26, sasa ni rasmi kuwa upo mashakani kwasababu Inter wanahangaika kupata Pauni milioni 40 ili kufikia masharti ya matumizi ya pesa waliyowekewa na Uefa. (Sun)
Kocha wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amesema beki kisiki na nahodha wa Ajax, Matthijs de Ligt, 19, anapaswa kujiunga na Manchester City msimu ujao. Nyota huyo pia anawaniwa na Barcelona na Man United. (Manchester Evening News)
De Ligt juma lililopita alitangaza kuwa uvumi juu ya yeye kujiunga na Man United inabidi upuuzwe.
Kocha wa Newcastle Rafael Benitez anapanga kusajili wachezaji wawili hivi karibuni kama klabu hiyo itanunuliwa na matajiri wa kiarabu kutoka Abu Dhabi. Wachezaji hao ni mshambuliaji kinda raia wa Venezuela Jan Hurtado, 19, anayechezea klabu ya Argentina ya Gimnasia La Plata pamoja na kipa wa Paris St-Germain Kevin Trapp, 28. (Daily Express)

RicharlisonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRicharlison

Kiungo wa Everton raia wa Brazil Richarlison, 22, amesema anafurahishwa kuhusishwa na kutaka kusajiliwa na klabu kongwe za Manchester United na Barcelona.(Teamtalk)
Uwezekano wa Barcelona kumsajili mshambuliaji wa Valencia Rodrigo Moreno, 28, umeongezeka maradufu. (Sport - in Spanish)

Rodrigo MorenoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRodrigo Moreno anakaribia kujiunga na Barcelona

Kiungo Mholanzi Kevin Strootman, 29, amesema klabu yake ya Marseille inataka kumpiga bei. (Corriere dello Sport - in Italian)
Kutokuimarika kiafya kwa beki wa Manchester City Eliaquim Mangala kumezima harakati za klabu yake ya zamani FC Porto ambao walikuwa wanataka kumrudisha Ureno Mfaransa huyo mwenye miaka 28. (A Bola - in Portuguese)

Eliaquim MangalaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEliaquim Mangala

Kocha wa Uholanzi Ronald Koeman amesema hatoikacha kazi yake ya sasa ili kujiunga na Barcelona iwapo klabu hiyo itaamua kumfurusha mkufunzi wake Ernesto Valverde. (De Telegraaf - in Dutch)

Tetesi Bora za Jumapili


Antoine Griezmann
Image captionAntoine Griezmann

Barcelona inataka kumsaini mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann, 28, na mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Juventus inajiandaa kulipa fidia ili kumnunua mkufunzi Maurizio Sarri kutoka Chelsea. (Independent)

Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPhilippe Coutinho

Chelsea itajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Brazil na Barcelona Philippe Coutinho, 26, iwapo wataondolewa marufuku ya kutosajili wachezaji. (Gianluca di Marzio)
Newcastle United yakanusha kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa AC Milan Gennaro Gattuso kama mkufunzi atakayerithi mahala pake mkufunzi wa sasa Rafael Benitez. (Newcastle Chronicle)

Gennaro Gattuso
Image captionGennaro Gattuso

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema kuwa ana kundi la WhatsApp la kibinafsi na Neymar na mchezaji mwenza Luis Suarez.
Arsenal itataka kumsaini beki wa kulia wa PSG mwenye umri wa miaka 27 Thomas Meunier. (Paris United)
download app ya MIKOGO BLOG playstore kwa taarifa zaidi
chanzo: bbc

Comments