Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 18.06.2019: Pogba, Bale, Lampard, Felix, Willian, Coutinho, Dembele

Frank Lampard


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kocha wa Derby Frank Lampard anajiandaa kukutana na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kujadiliana kuhusu uwezekano wake kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Maurizio Sarri. (Sun)
Chelsea wanataka kumpatia Lampard,40, mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja wa Stamford Bridge. (ESPN)
Bayern Munich haijawasiliana na winga wa Real Madrid Gareth Bale,29, anasema wakala wa nyota huyo wa kimataifa wa Wales. (ESPN)
Manchester United midfielder Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Manchester United inapania kumlipa Paul Pogba, 26, hadi pauni nusu milioni (£500,000) kwa wiki licha ya Real Madrid na Juventus kumnyatia kiungo huyo raia wa Ufaransa. (Mail)
Benfica imepuuzia tetesi kuwa Atletico Madrid itaipiku Manchester City katika usajili wa mshambuliaji wa Ureno, Joao Felix, 19 kwa kima cha pauni milioni £107 na kuzitaja tetesi hizo kuwa "taarifa feki". (AS)
Joao FelixHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJoao Felix
Chelsea wamekataa dau la pauni milioni £35 kutoka kwa Barcelona na Atletico Madrid la kumnunua mshambuliaji wa miaka 30 Mbrazil Willian. (Sky Sports)
Paris St-Germain wanataka kukamilisha mchakato wa usajili wa mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, baada ya michuano ya Copa America. (AS)
Coutinho pia analengwa na Manchester United lakini huenda asiwasikilize kutokana na heshima alionayo kwa klabu yake ya zamani ya Liverpool. (Sky Sports)
Philippe Coutinho points to his ears after scoring against Manchester UnitedHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Liverpool wamepewa ishara ya kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, wa Barcelona endpo wataweza kulipa pauni milioni 90. (TEAMtalk)
Crystal Palace wamekataa dau la pauni milioni 50 lililotolewa na Manchester United kumnunua beki wake wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 21. (Sky Sports)
United pia wamepoteza matumaini ya kumsajili mlinzi wa West Ham Issa Diop baada ya dau lao la pauni milioni £40m kukataliwa.
Mkataba huo ulihusisha mmoja wa wachezaji wa United kujiunga na klabu hiyo japo haijabainika ni mchezaji yupi. (Telefoot, via Metro)
Issa DiopHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMlinzi wa West Ham Issa Diop
West Ham wameiambia Eibar kuwa wako tayari kulipa ada ya pauni milioni £13.4 kugharimia uhamisho wa kiungo wa kati wa Uhispania Joan Jordan. (Marca)
Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumsajili upya beki wa kushoto wa PSV Eindhoven Mhispania Angelino, Mwaka mmoja baada ya kumuuza kiungo huyo wa miaka 22. (Sun)
Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano ya  mkataba mpya na kiungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 31. (Mirror)
Juan MataHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMata alitua Old Trafford Manchester United ikiwa chini ya ukufunzi wa kocha wa zamani David Moyes
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, ameambiwa na kocha wa timu ya taifa yake ya taifa Roberto Martinez kwamba "hana budi kuondoka Manchester United". (Het Laatste Nieuws - in Dutch)
Mshambuliaji wa Chelsea muingereza Martell Taylor-Crossdale,19 anafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Hoffenheim kwa mkataba wa kudumu. (Sky Sports)

Tetesi Bora Jumatatu

Klabu ya Paris St-Germain ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake machachari raia wa Brazil, Neymar, 27. (L'Equipe - in French)
NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNeymar alijinga na Barcelona kutoka Santos mwaka 2013
Klabu ya Bayern Munich inataka kumsajili kwa mkopo winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale, 29. (Sun)
Kiungo wa klabu ya Lyon Mfaransa Tanguy Ndombele, 22, amesema kuwa anaweza kuhamia Tottenham kama nafasi itatokea. (Telefoot - in French)
Winger wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza kujiunga na Chelsea. (Express)
CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPhilipe Coutinho amekuwa akihusishwa na fununu za kuhama klabu ya Barcelona
Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kufukuzia saini ya kiungo wa klabu ya Besiktas na Uturuki, Dorukhan Tokoz, 23. Tayari ofa ya klabu ya Udinese ya Italia ya kutaka kumsaini kiungo huyo imekataliwa na Besitkas. (Fotomac - in Turkish)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsajili kipa wa klabu ya Eibar Mhispania Asier Riesgo, 35. (Sun)
Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi ameonya kuwa hataki tena kuona "tabia za watu mashuhuri" kutoka kwa wachezaji wake. (France Football - in French)
chanzo: bbc

Comments