Tangazo la Ajira

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sinai Healthcare Polyclinic ni taasisi mpya inayotoa huduma za kitabibu, inayoongozwa na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu pamoja na timu za watoa huduma wengine. Katika kuboresha huduma kwa wateja, Sinai Healthcare Polyclinic inatangaza nafasi mpya za kazi kama ifuatavyo: –
Laboratory technician 1 post
Sifa za muombaji
Muombaji awe ni muhitimu wa stashahada (diploma) ya maabara kutoka katika chuo kinachotambulkika na NACTE na awe amesajiliwa na baraza husika la kitaaluma.
Assistant laboratory technician 1 post
Sifa za muombaji
Muombaji awe ni muhitimu wa astashahada (certificate) ya maabara kutoka katika chuo kinachotambulkika na NACTE na awe amesajiliwa na baraza husika la kitaaluma.

Pharmaceutical technician 1 post
Sifa za muombaji
Muombaji awe ni muhitimu wa stashahada (diploma) ya pharmacy kutoka katika chuo kinachotambulkika na NACTE na awe amesajiliwa na baraza husika la kitaaluma.
Assistant pharmaceutical technician 1 post
Sifa za muombaji
Muombaji awe ni muhitimu wa astashahada (certificate) ya pharmacy kutoka katika chuo kinachotambulkika na NACTE na awe amesajiliwa na baraza husika la kitaaluma.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
i. Muombaji alete barua yake ya maombi katika benchi la mapokezi, Sinai Healthcare Polyclinic, Boko Basihaya, Tegeta – Dar es Salaam.
ii. Barua zote ziambatanishwe na nakala za cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo ikiwemo sekondari pamoja na vyeti vya kitaaluma.
iii. Muombaji aoneshe nafasi anayoomba nje ya bahasha ya barua ya maombi
iv. Muombaji aambatanisha CV yake yenye majina na mawasiliano ya referees wawili.
v. Watu wachache tuu wataitwa kwaajili ya usaili.
vi. Wasiliana nasi kupitia namba ya simu ya mkononi: 0754 490468

Comments