Mwanachama wa Yanga Bilionea Rostam Aziz amesema yuko tayari kuwapeleka nje ya nchi viongozi wa Yanga ili wakapate mafunzo ya uendeshaji wa klabu hiyo kwa kutumia mfumo usiokuwa tegemezi
Rostam aliyeichangia Yanga Tsh Milioni 200, amepinga mfumo wa uendeshaji wa timu ambao utamtegemea mtu mmoja au ufadhili kwani amesema mfumo huo utawanyima sauti wanachama ambao ndio wenye timu
Katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam leo, Rostam alisema atawasilisha mapendekezo yake kwa uongozi wa Yanga katika kikao ambacho amepanga kukutana nao
"Nipo tayari kuwapeleka nje viongozi wa Yanga SC ili wakapate mafunzo kutoka kwa wataalamu namna ya kuendesha klabu pia wakihitaji ntawaleta hapa hapa wataalamu," alisema
"Napenda kuona Yanga inafanikiwa kupitia umaarufu na idadi kubwa ya wanachama iliyonayo , kutomilikiwa na mtu mmoja kutatoa fursa kwa makampuni mengine mengi kuidhamini"
"Nami ntaangalia kupitia moja ya makampuni Yangu kutangaza bidhaa zake kupitia Yanga, pia nitakaribisha makampuni mengine kufanya hivyo"
Comments
Post a Comment