Mzee wa miaka 70 akamatwa kwa 'kulipiga mawe' gari la Rais


MuseveniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais wa Uganda Yoweri Museveni
Mzee wa miaka 70 amekamatwa nchini Uganda kwa tuhuma za kulipiga mawe gari ya Rais Museveni likiwa kwenye msafara mwaka jana.
Mzee Omar Risasi Amabua alikamatwa katika Mji wa Arua na baadaye kuhamishiwa katika mahabusu iliyoko Gulu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nile Magharibi, Christopher Barugahare mtuhumiwa huyo atashtakiwa kwa uhaini.
"Tumemkamata kwa sababu amehusishwa na tukio la mwaka jana ambapo gari la rais lilishambuliwa kwa mawe," Bw. Barugahare alisema.
Gari hilo lilishambuliwa Augosti 13, 2018, siku ya mwisho wa kapeini za uchaguzi mdogo wa Manispaa ya Arua.
Gari la Rais MuseveniHaki miliki ya pichaTWITTER
Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia mauaji ya kinyama ya Mbunge Ibrahim Abiriga na mlizi wake ambaye alitajuw akuwa ndugu yake.
Tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza vitengo vya usalama kuwatafuta wauaji wa kiongozi huyo .
Abiriga ambaye masomo yake yalitiliwa shaka na wapinzani wake alikuwa mgombea wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM)
Kampeini ya kumuondoa kitini ilikumbwa na ghasia siku ya mwisho baada ya mwana chama wa Forum for Democratic Change, Kassiano Wadri, kuamua kuwania kiti hicho kama mgombea huru kuonesha dalili ya kushinda uchaguzi huo. Wadri alishinda uchaguzi kama ilivyobashiriwa.
Rais Museveni alikuwa mjini Arua, siku ya mwisho ya kampaini ya uchaguzi mdogo, kumpigia debe mgombea wa NRM Nusura Tiperu, ambaye alishindwa katika uchaguzi huo na hata rufaa aliyowasilisha mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo kutupiliwa mbali.
Kizza Besigye kuhusu muungano wa kisiasa na Bob Wine
Msafara wa rais ulikutana na wafuasi wa Wadri ambao walikuwa wakiimba nyimbo zilizo na ujumbe wa kuunga mkono vyama vinavyoegemea mrengo wa upinzani.
Kwa mujibu wa maafisa wa Ikulu na maafisa wa polisi, gari lililokuwa limebeba mzigo wa rais ilipigwa mawe na wafuasi wa upinzani, jambo ambalo halikubaliki..
Hali ambayo ilivifanya vikosi vya usalama kuingolia kati kutuliza mambo.

Watu 36 walikamatwa miongoni mwao wabunge na wanahabari.
Yasin Kawuma, ambaye ni dereva wa mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine alipigwa risasi na kuuawa.
Wabunge Wadri, Bobi Wine na mwenzake wa manispaa ya Mityana Bw.Francis Zaake, pamoja na watu wengine 31 wameshtakiwa kwa kosa la uhaini kufuatia madai ya kushambuiwa kwa msafara wa rais.
source: bbc

Comments