Marlaw aibuka kwenye show ya Diamond Kahama,Asema amempa HAMASA.



Unakumbuka nyimbo kama Rita na Pipii zilizotamba hapo nyuma, bila shaka huwezi kumsahau aliyekua nyuma ya hit songs hizo ambaye anafahamika kwa jina la Marlaw.
Msanii huyu kwasasa yuko kimya sana na ni zaidi ya miaka minne tangu mara ya mwisho kuonekana kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi alipokuwa akitumbuiza kibao chake cha “pipii” alichokigeuza kwa kukisifia chama hicho kikongwe barani Afrika mwaka  2015.
Marlaw akihojiwa na Wasafi TV mjini kahama jana amedai kuwa sababu ya yeye kuwa kimya kunatokana na changamoto za kimaisha zilizomtokea “Kumekuwa na mambo mengi..changamoto za maisha” amedai kuwa licha ya changamoto hizo zimemfanya kuwa imara zaidi “me nadhani ilikua nikujiandaa zaidi” na anaamini changamoto alizopitia ambazo hakuzitaja zilikua kwa lengo zuri “ilikua kwa lengo zuri ” nimekaa kimya kwa lengo zuri”
March 2011 msanii huyo alimuoa msanii mwezake wa Bongo Fleva, Besta na mwaka 2016 walifanikiwa kupata mtoto wa tatu.Awali iliripotiwa kuwa wawili hao kuachana mwaka 2015 mpaka pale ilipokuja kukanushwa na Besta alipozungmza na kituo cha redio cha Clouds Fm.
Kwasasa Marlaw anaishi mjini Kahama  anapokaa na wazazi wake ambapo hapo awali alikua anakaa wilayani Maswa na siku ya jana nae alijitokeza kutoa surport kwa kuhudhuria show ya One Man One Mic ya Diamond Platnumz iliyofanyika katika viwanja vya Taifa “nimekuja kwasababu ya kumsuport …kilichonileta kingine ni mashabiki zake ..wamenipa msukumo”imempa mzuka
Mara ya mwisho Marlaw alifanya wimbo na producer wa muziki nchini Fundi Samweli iliyokuwa inakwenda kwa jina la “Pamoja” mwaka 2016 kazi ambayo haikufanya vizuri sokoni.
Pia Marlaw amedai kuwa alichokifanya Diamond Platnumz katika show ya Kahama kimempa hamasa kubwa sana na anajiandaa kutoa hit song ambazo zitasikika hivi karibuni “mziki naanza tena sasa hivi naamini ntafanya vizuri” Cheki hapa full interview aliyoifanya na Wasafi TV.

Comments