Mama aiomba mahakama isimuue baba aliyewaua watoto wake watano

Amber Kyzer


Haki miliki ya pichaCBS
Image captionIwapo ningekuwa na uwezo wa kuurarua uso wake ningeurarua alisema Amber Kyzer
Mama mmoja wa watoto watano waliouawa na baba yao amelitaka jopo linalosikiza kesi ya mumewe kutomwekea hukumu ya kifo.
Amber Kyzer aliiambia mahakama moja huko Carolina ya kusini kwamba Tim Jones Jr hakuwaonea huruma wanangu kwa njia yoyote ile lakini wanangu walimpenda sana.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 37 alihukumiwa mwezi Mei kwa kuwauawa watoto wake wenye umri kati ya mmoja hadi nane, nyumbani kwake karibu na Lexington mnamo tarehe 29 Agosti 2014.
Jopo hilo linajadiliana iwapo Jones anafaa kupewa kifungo cha maisha ama kunyongwa. ''Nasikia kile ambacho watoto wangu walipitia'', alisema bi Kyzer katika mahakama siku ya Jumanne.
''Na kama mama iwapo ningekuwa na uwezo wa kuupasua uso wake ningeupasua. Hicho ndio nilicho nacho ndani yangu''.
Timothy Ray Jones awasilishwa mahakamaniHaki miliki ya pichaCBS
Image captionTimothy Ray Jones akionekana katika mahakama ya Lexington tarehe 4 mwezi Juni
Bi Kyzer aliliambia jopo hilo kwamba alikuwa akipinga hukumu ya kifo kwa kipindi chote cha miasha yake
Alisema kwamba licha ya kutamani sheria 'imkaange' mumewe asingepenedelea kumchagulia hukumu ya kifo.
''Hakuwaonyesha watoto wangu huruma yoyote'' , alisema. ''Lakini watoto wangu walimpenda na iwapo ninazungumza kwa niaba yangu na watoto wangu basi hilo ndio tamko langu''.
Bi Kyzer hata hivyo alisema kwamba ataheshimu chochote kitakachotolewa na jopo hilo la majaji.
Alikuwa ameitwa kutoa ushahidi wake na mawakili wa mumewe.
Wanandoa hao walifunga ndoa wiki sita baada ya kukutana 2004, wakati wote walipokuwa wakifanya kazi katika bustani ya watoto ya kucheza katika eneo la Chicago
Watoto wote watano waliuawa na baba yaoHaki miliki ya pichaCBS
Image captionJones aliendesha gari kwa siku tisa mabaki ya watoto hao yakiwa ndani ya gari lake
Lakini alitoa ushahidi mwezi Mei kwamba ndoa yao ilikuwa imekumbwa na mushkeli kwa kuwa alikuwa na masharti mengi na kwamba 'wanawake hawakutakiwa kusikika bali kuonekana pekee'.
Walipotengana baada ya miaka tisa alimpatia watoto aishi nao kwa sababu alikuwa akifanya kazi iliokuwa ikimpatia pato la $80,000(£63,000) kwa mwaka.
Mwanamke huyo alikuwa akiwaona watoto hao kila Jumamosi katika mgahawa mmoja.
Siku ambayo Jones aliwaua watoto hao, mahakama iliambiwa kwamba alikasirika alipomuona mtoto mwenye umri wa miaka sita Nahtan akicheza na plagi ya umeme nyumbani.
Alimuua mvulana huyo na baadaye kuwanyonga watoto wengine wanne-Elaine, Gabriel, Elias na Mera.
Jones baadaye aliifunga miili yao kwenye mfuko wa plastiki, jopo hiyo liliambiwa, na kuiweka ndani ya gari moja na kuondoka kwa siku tisa kabla ya kuacha mabaki hayo katika jimbo la Alabama.
Alikamatwa katika kituo kimoja cha traffiki mjini Missisipi wakati maafisa wa polisi walipotambua harufu iliokuwa ikitoka ndani ya gari hilo.
Jones alikana kuhusika na mauaji ya watoto hao alipofikishwa mahakamani.
Upande wa mshukiwa ulisema kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiakili ambao pia ulimwathiri mamake.
Wanasema kuwa aliathirika baada ya mkewe wake kumtoroka na kuanza uhusiano na kijana mmoja jirani.
chanzo: bbc

Comments