ZAERA KUSAJIRI NANE KABLA YA MAY 29

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo May 29 2019 kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya Taifa ya nchi hiyo, yeye akiwa kocha Msaidizi


Yanga itacheza na Azam Fc May 28 mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu na baada ya mchezo huo Zahera ataondoka usiku


Zahera amesema DR Congo inakwenda kuweka kambi Hispania kujiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika Misri kuanzia Juni 21 2019


Mcongoman huyo amefichua kuwa kabla ya kuondoka atakamilisha usajili wa nyota saba au nane


Comments