Licha ya kutofanya mazoezi, kikosi cha Yanga leo kimepambana na kuweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zimeharibu uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini ambao unatumiwa na Yanga
Baada ya kurejea kutoka Musoma ambako ilicheza na Biashara United, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja.
Lakini walishindwa kufanya mazoezi baada ya mapumziko hayo, mvua ikitajwa kuwa kikwazo
Hata hivyo, wachezaji wa Yanga leo wamepambana kupata ushindi ambao ni zawadi kwa uongozi mpya wa timu hiyo
Kocha Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji kwa juhudi zao zilizofanikisha kupata ushindi
Yanga haikuwa imeshinda tangu kuingia kwa uongozi mpya chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla wakipoteza michezo dhidi ya Lipuli na Biashara United
Uongozi mpya umeweka mkakati wa kuhakikisha Yanga inashinda michezo yote iliyobaki
Comments
Post a Comment