Yanga yafuta mpango wa Simba wa kukabidhiwa ubingwa May 23
Ushindi wa bao 1-0 wa Yanga dhidi ya Ruvu Shooting leo, umefuta ndoto za Simba iliyotaka kukabidhiwa ubingwa wa ligi kuu May 23 itakapocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla
Yanga imefikisha alama 83 na itaweza kufikisha alama 89 kama itashinda michezo miwili iliyobaki
Kabla ya May 23, Simba inakabiliwa na michezo miwili dhidi ya Mtibwa Sugar na Ndanda Fc hivyo hata kama itashinda yote haitakuwa imetwaa ubingwa kwani itafikisha alama 88
Yanga itashuka tena dimbani May 22 kucheza na Mbeya City mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Hivi karibuni Afisa Habari wa Simba Haji Manara alifichua mpango wa timu hiyo kuomba kukabidhiwa kombe May 23 akiamini wataweza kushinda michezo yote mitano iliyokuwa imepangwa kupigwa uwanja wa Uhuru
Hata hivyo mpango huo hautawezekana tena
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesema hata kama Simba ingeweza kushinda michezo yake isingekabidhiwa kombe kwa kuwa kanuni haziruhusu
Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kulingana na kanuni za uendeshaji wa ligi, bingwa atakabidhiwa kombe katika mchezo wa ligi kuu na si vinginevyo
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alikosoa mpango huo uliowekwa hadharani na msemaji wa Simba, akibainisha tukio hilo ni ishara kuwa Simba iliandaliwa kupewa kombe na sio kutwaa ubingwa msimu huu
Comments
Post a Comment