Baada ya mchezo dhidi ya Biashara United jana, kikosi cha Yanga kinarejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa Jumatatu, May 13 katika uwanja wa Uhuru
Baada ya kupoteza mchezo wa jana, Yanga ni kama haina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu, kilichobaki ni kukamilisha ratiba tu
Kihamesabu, Simba inahitaji kushinda michezo mitatu tu ili iweze kutetea ubingwa, huku wakiwa na michezo sita ya viporo
Baada ya mchezo wa Ruvu Shooting, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Mbeya City kisha kumaliza msimu kwa kuumana na Azam Fc
Kocha Mwinyi Zahera amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti waliyotoa tangu mwanzoni mwa msimu na ameahidi msimu ujao watarejea wakiwa imara zaidi
Comments
Post a Comment