Yanga iko mbioni kukamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Mukura Victory, Patrick Sibomana ambaye tayari yuko jijini Dar es salaam kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria
Sibomana mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Mukura Victory mwezi Disemba mwaka jana akitokea barani Ulaya alikokuwa akikipiga Shakhtyor Soligorsk ya Belarus
Winga huyo pia amewahi kuichezea APR mwaka 2017
"Ndiyo nakwenda kumaliza mipango ya kuichezea Yanga, tutazungumza wakinipatia vile ni navyotaka nitasaini mkataba, na msimu ujao nitacheza Tanzania, " Sibomana amenukuliwa na Bin Zubeiry
Comments
Post a Comment