Wafaransa watatu wahukumiwa kunyongwa huko Iraq

A member of the Iraqi rapid response forces walks past a wall painted with the black flag commonly used by Islamic State militants, at a hospital damaged by clashes during a battle between Iraqi forces and Islamic State militants in the Wahda district of Mosul, Iraq,

DW imeripoti kuwa Mahakama moja nchini Iraq jana Jumapili iliwahukumu adhabu ya kifo raia watatu wa Ufaransa waliokuwa wanachama wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Raia hao walikamatwa nchini Syria na vikosi vinavyoungwa mkono na Marekani vinavyopambana na wanajihadi na kisha kupelekwa nchini Iraq. Kevin Gonot, Leonard Lopez na Salim Machou wana siku 30 za kukata rufaa kuhusiana na hukumu hiyo. Mahakama ya Iraq ilisema mapema mwezi huu kwamba imewahukumu zaidi ya wageni 500 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa IS tangu mwaka 2018. Hukumu hiyo imekosolewa na makundi ya haki za binadamu. Raia hao 3 waliohukumiwa jana ni miongoni mwa wafaransa 13 waliokamatwa katika mapambano huko mashariki mwa Syria na kukabidhiwa kwa mamlaka za Iraq mwezi Februari. Iraq ilitangaza kuliangamiza kundi la IS mwishoni mwa mwaka 2017 na kuanza kuwashitaki wageni waliodaiwa kujiunga na kundi hilo. Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International, Iraq ndio nchi inayoongoza katika utekelezaji wa adhabu ya kifo duniani.

Comments