"Simba walikuwa na michezo 12 ya viporo. Walikuwa wanafahamu matokeo ambayo wanatakiwa wapate ili watwae ubingwa, pengine hali ingekuwa tofauti kama wangecheza sambamba na timu nyingine," amesema Rajabu Issa kutoka Buguruni
"Umeona wapi na ligi gani duniani ambapo timu moja inakuwa na michezo ya viporo 12? kushiriki ligi ya mabingwa haitoshi kuwa sababu ya kurundikiwa michezo mingi kiasi hicho mbona timu walizokuwa wakishindana nazo zilikuwa zikicheza ligi zao?"
"Hawa Simba baada ya kutolewa kombe la FA walipanga mkakati na TFF kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi kuu kupitia ratiba na hujuma kwa Yanga"
"Angalia mchezo dhidi ya KMC ilikuwa wafungwe lakini refa akawatafutia ushindi kwa nguvu halafu baadae TFF wanatangaza kumfungia mwamuzi wakati mpango umeshakamilishwa"
Comments
Post a Comment