Mahakama ya ngazi ya juu zaidi nchini India imetoa jibu la swali hilo na kusema kuwa ni "ndio".
Katika uamuzi muhimu, mahakama imepitisha uamuzi wa mahakama ya awali na kumtia hatiani daktari kwa kosa la ubakaji katika jimbo la lati la India la Chhattisgarh kwasababu alikuwa na makibaliano ya ya uhusiano wa kingono na mwanamuke baada ya kumuahidi kuwa atamuoa, lakini baadaye hakutimiza ahadi hiyo na kumuoa mtu mwingine.Majaji L Nageswara Rao na MR Shah walisema mwanamke alimruhusu daktari kufanya ngono naye kwasababu aliamini kuwa daktari alikuwa na lengo la kumuoa kwa hiyo haiwezi kuchukuliwa kuwa alimruhusu kufanya tendo hilo la ngono kwa hiari.
Bado India ni taifa lenye itikadi za kihafidhina linapokuja suala la ngono na mambo yanayohusu jinsia kwa ujumla.Mabikra huzawadiwa na mwanamke anayejulikana kuwa aliwahi kufanya tendo la ngono nje ya ndoa huwa inakuwa vigumu kwake kuolewa.
Majaji walisema kuwa mshtakiwa alikuwa na "lengo la wazi " la kutomuoa , na kuongeza kuwa "tendo la ngono linalofanyika bila dhana halisi haliwezi kuchukuliwa kama hiari ".hata hivyo mahakama ilipunguza kifungo cha miaka 10 alichokuwa amefungwa na mahakama ya mwanzo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka 7 jela , majaji wamesema kuwa ''nilazima akabiliwe na athari za uhalifu alioutekeleza ".
Hii si kesi ya kwanza - kwa mujibu wa data za serikali za mwaka 2016, polisi walirekodi kesi 10,068 za aina hiyo za ubakaji ''zinazofahamika kama za waathiriwa wa ahadi ya kuolewa". Mwaka 2015, idaidi ya kesi hizo zilikuwa ni 7,655.Majaji wa mahakama ya juu zaidi walizishauri mahakama za mwanzo "kuchunguza kwa makini ikiwa kweli mwanamume aliahidi kumuoa muathiriwa au kulikuwa na njama nyingine tangu mwanzo na kwamba alifanya tendo la ngono kwa lengo tu la kuridhisha nafsi yake''.
Hii ina maana kuwa kama mwanaume atathibitisha kuwa kweli alitaka kumuoa mwanamke lakini akabadili nia hiyo baadae , bado haitakuwa ubakaji. Haichukuliwi kama ubakaji ikiwaitabainika kuwa alikuwa na njama mbaya tangu mwanzoni mwa mahusiano yao.
Lakini kama kweli tendo hilo lilifanyika kwa "lengo fulani " si rahisi kuthibitisha, na uamuzi huachiwa majaji na pia kuna hofu kuwa sheria hiyo inaweza kutumiwa isivyotarajiwa.
Na ukweli ni kwamba ,kutokana na idadi kubwa ya kesi hizo, Jaji Pratibha wa Mahakama ya juu ya Delhi mwaka 2017 alisema kuwa wanawake hutumia sheria za ubakaji wakati wanapokuwa na mahusiano mabaya ya ndoa.
chanzo: bbc
Comments
Post a Comment