SIKU YA KUICHANGIA YANGA KESHO

Tukio maalum la futari na chakula cha jioni 'Gala Dinner' litafanyika kesho May 18 licha ya taarifa iliyotolewa awali na Mwenyekiti wa Yanga kuwa tukio hilo limeahirishwa


Taarifa iliyotolewa na Yanga leo imebainisha kuwa tukio hilo litafanyika kesho Jumamosi, May 18 2019 Hotel ya Serena jijini Dar es salaam kama ilivyotangazwa awali


Wageni mbalimbali wakiwemo viongozi na wananchi wa kawaida ambao ni wadau wa Yanga wamealikwa kwenye tukio hilo la kihistoria


Yanga imedhamiria kutumia hafla hiyo kukusanya fedha za kutosha katika mkakati wake wa kukusanya Bilioni 1.5, fedha za usajili


Comments