Reginald Mengi afariki dunia Leo!


Image result for reginald mengi photos

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi amefariki dunia.
Taarifa hiyo imethibitishwa leo alfajiri na vyombo vya habari vilivyo chini ya umiliki wake, runinga ya ITV, na stesheni ya Radio ONE.
 Mengi alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro na umauti umemkuta akiwa mjini Dubai, Falme za Kiarabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ameongoza mamilioni ya Watanzania kutuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huo.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter Magufuli amesema ataendelea kumkumbuka Mzee Mengi kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa lake.
Salamu za rambirambi pia zimetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbas ambaye amenukuu kauli ya marehemu Mengi kuwa; " 'watu wanaoacha alama hawafi', basi mawazo, falsafa, ubunifu na kujitoa kwake vitaendelea kuishi nasi."
Waziri wa zamani wa Habari nchini Tanzania Nape Nnauye naye ametumia ukurasa wake wa Twitter kuelezea masikitiko yake juu ya kifo cha mtu aliyemuita kuwa ni 'rafiki, mshakaji, kiongozi na mzazi.'
"Ulinifundisha kuwa kukata tamaa ni dhambi," ameandika Nnauye.

Comments