Polisi ya kupambana na ghasia nchini Indonesia imefyatua mabomu ya gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji katikati ya mji mkuu Jakarta, wakati makabiliano mapya yalizuka katika mitaa ya mji huo kufuatia tangazo la matokeo rasmi ya uchaguzi.
Waandamanaji waliwarushia polisi fashifashi na kuwasha moto kwenye mojawapo ya barabara kuu karibu na ofisi ya tume ya uchaguzi wakati wakijaribu kuvunja mzingiro wa nyaya uliowatenganisha na polisi. Kumekuwa na matukio ya fujo za hapa na pale mjini Jakarta tangu Jumanne,
wakati tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Rais Joko Widodo amempiku mpinzani wake mkuu jenerali wa zamani Prabowo Subianto katika uchaguzi wa Aprili 17. Watu sita wameripotiwa kuuawa katika makabialiano hayo ya polisi na waandamanaji.
chanzo: DW
Comments
Post a Comment