Wakati Gadiel Michael akiendelea kuuguza majeraha ya kifundo cha mguu, Yanga itamkosa beki wake Abdallah Shaibu 'Ninja' katika mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Hata hivyo nyota Mrisho Ngasa na Andrew Vicent waliokosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, wanatarajia kurejea kikosini
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri wakiendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo
"Jana tumefanya mazoezi ya kujitoa uchovu leo yanaendelea lakini kikosi kipo vizuri tunaamini ushindi utapatikana," amesema
Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 83, alama tano nyuma ya Simba inayoongoza ligi
Simba inaweza kutwaa ubingwa leo mkoani Singida kama itapata ushindi au kupata matokeo ya sare. Simba inahitaji alama moja tu
Matokeo ya michezo miwili iliyobaki hayawezi kuathiri nafasi ya pili ya Yanga kwenye msimamo wa ligi
Azam Fc inayoshika nafasi ya tatu, haiweze kuifikia Yanga hata kama itashinda michezo miwili iliyobaki
Comments
Post a Comment