
Mchekeshaji maarufu Afrika mashariki Eric Omondi amewachana na mpenzi wake wa siku nyingi Chantal Grazioli.
Uvumi wa kuvunjika kwa penzi lao la miaka minne ulisambaa katika mitandao ya kijamii kabla ya Omondi mwenyewe kuthibitisha rasmi katika mtandao wake wa Instagram.
Tukio hilo linajiri wakati ambapo mchekeshaji huyo anazidi kuvutia mashabiki wengi katika sekta hiyo ya uchekeshaji huku wengi wakihoji ni nini haswa kilichosababisha kuvunjika kwa mahaba yao.
Katika chapisho lake refu katika mtandao huo wa Instagram, Omondi ameandika kwamba anamtakia heri Grazioli huku akiendelea na awamu yake mpya ya maisha bila yeye huku akisisitiza kuwa mwanadada huyo alibadilisha maisha yake.
''Nilikutana nawe ukiwa na umri wa miaka 19.... Nimekuwa kwa miaka minne na nusu....tuliishi na kuwa na wakati mzuri zaidi katika maisha naye. Ulibadilisha maisha yangu kabisa....wakati unapoanza maisha yako mapya na mimi au bila mimi nakutakia heri mpenzi wangu. Njia iliotuleta pamoja sasa inatupeleka maeneo tofauti na unapoenda njia tofaut nakutakia heri katika maisha'', aliandika.
Na kutokana na visa vingi vya uhalifu wa kimapenzi...Eric Omondi alitoa ushauri wa bure kwa wanaume kuhusu jinsi wanavyotakiwa kufanya kufuatia kuvunjika kwa mahusiano yao na wapenzi wao.
CHANZO:BBC
Comments
Post a Comment