Mbunge huyu anataka Bangi iruhusiwe Tanzania

 
Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba anataka serikali kuhalalisha matumizi ya bangi ama marijuana nchini tanzania kwa mautumizi ya dawa.
Aliambia bunge siku ya Jumatatu kwamba mataifa mengine manne ya Afrika tayari yemahalalisha Marijuana kutumiwa kutengeneza dawa.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania mbunge huyo anasema kuwa ni vyema kama taifa kuanza kufikiria kuhusu fursa hiyo mapema.

''Tunavyozungumza, Uganda imehalalaisha upanzi wa Marijuana kwa matumizi ya dawa'', alisema akitaja ripoti za hivi majuzi kwamba taifa hilo la Afrika mashariki limenunua mbegu kupanda mmea huo.

''Sijui ni kwa nini kitengo cha chakula na dawa hakijachukua sampuli kuelezea serikali kwamba dawa hizo zina bangi ndani yake'', alihoji.

bonyeza hiyo link hapo chini kupata APP yetu 
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.mikogo.blog

Comments