Mambo usiyoyafahamu kuhusu Reginald Mengi


Image result for reginald mengi

Tanzia imeligubika Taifa la Tanzaniai baada ya kumpoteza mwana msomi na mfanya biashara maarufu ambaye ni mmojawapo wa watu matajiri zaidi barani Afrika.
Hatahivyo ni wachache wanaojua alichopitia mfanyibiashara huyo kabla ya kuwa mtu tajiri hadi kifo chake.
Haya hapa mambo saba ambayo marehemu alipitia na kuyafanya katika maisha yake.

1. Alilala sakafuni

Safari ya  bwana Mengi ilianzia eneo la Machame huko Kilimanjaro ambako alidaiwa kulala chini na ng'ombe.
Wazazi wake walikuwa wakulima huku akidai kwamba elimu ya msingi kuhusu ujasiriamali aliitoa kwa mamake.
Mengi anasema mamake alikuwa akichukua mkungu wa ndizi na kurudi nyumbani na kilo ya mchele mara nyengine alichukua kuku mmoja pekee na kurudi na mfuko wa viazi.
Mara nyingi alichukua mikungu ya ndizi na kuja na sare ya shule.
2. Alitoroka Shule
Alipokuwa kidato cha tano nchini Tanzania alipata fursa ya kusomea uhasibu katika chuo kikuu huko Glasco nchini Uskochi na kutokana na usiri wake mkubwa hakumuelezea mwalimu wake mkuu kwamba ameshinda ufadhili wa masomo huko uskochi.Kwa hiyo alitoroka shule licha ya kila mtu kujaribu kumshawishi kukaa.

3.Aliwahi kuwa kondakta wa basi

Alipokuwa shuleni huko Glasgow, mengi alibadilisha mawazo kwa kile alichosomea kwa kuwa hakutaka kuwa karani tena.

Wadhamini wake walisema kuwa alifaa kusalia uskochi kwa miezi sita kwa kuwa walikuwa wamelipia karo muda huo wote.
Alikaa lakini aliacha masomo na badala yake akaamua kumalizi masomo ya mbele akisoma usiku tu huku wakati wa mchana akifanya kazi nyingi kutoka kuwa kondakta wa basi hadi kuwa mfanyakazi wa usafi.

4.Alijiuzulu saa chache baada ya kupewa kazi Kenya

Baada ya kumaliza masomo yake Coopers brothers ambao ndio Prize Waterhouse Coopers PCW walimuajiri Mengi.
Alipanda hadi kufikia cheo cha juu kabisa kabla ya kuwa mwanachama wa taasisi ya uhasibu ya Uingereza na Wales lakini akatamani kurudi nyumbani.
Baada ya miaka tisa Mengi alihamishwa hadi ofisi ya Nairobi lakini baada ya saa chache tu akiwa Kenya alijiuzulu.

5.Alikuwa na bidii ya mchwa

Alisema nilitamani kurudi Tanzania licha ya kujua kwamba ningetajirika iwapo ningesalia Uingereza.
Lakini nilitaka kurudi nyumbani ili kuwafanyia kitu watu wangu. Baada ya mwaka mmoja akiishi Moshi mengi alihamia Dar es salaam akaajiriwa tena na PWC.
Alifanya kazi kwa bidii na akiwa na umri wa miaka 30 alikuwa mmoja wa washirika wadogo sana katika shirika hilo.
Lakini kwa mara nyingine akiwa na PWC Mengi alikuwa mwenyekiti na meneja mwenza alijiuzulu.

6. Aliulaumu mfumo wa Ujamaa Tanzania na kuanza kuuza kalamu

Katika mahojiano yaliochapishwa na jarida la Forbes Afrika Mengi alisema kuwa ndoto yake ilikuwa kuendesha biashara kubwa na kwamba aliulaumu mfumo wa ujamaa kwa kuwa uliua wajasiriamali.
Mwaka 1980 kulikuwa na uhaba mkubwa kutokana na serikali kuendeleza sera ambazo zilipendelea bidhaa za ndani.
Ulikuwa uhaba huo huo ambao ulimfanya bwana Mengi kwenda katika biashara miaka 1980's.
Akiunda na kuuza kalamu. Alikuwa akiagiza vifaa kutoka Kenya na kutengeza kalamu hizo chumbani mwake.
Biashara hiyo ya kalamu ndio iliokuwa mwanzo wake wa kuingiza dola milioni moja.
7Mara ya kwanza alikataliwa na Jacqueline Ntuyabaliwe
Mengi anasema haikuwa rahisi kumpata mkewe , kwani mara ya kwanza alipomtaka kuonana naye binti huyo wakiwa Ulaya alikataa.
Anasema aliendelea kumfuata na waliporudi nchini Tanzania ndipo sasa wakaonana na penzi likaanza kunoga.
Mengi anasema kuwa iwapo asingekuwa na mpenzi huyo labda angekuwa amefariki.
katika kitabuu chake I can , I must, I will, mengi anamzungumzia mrembo huyo kama aliyeleta mwangaza maishani mwake.
Ananipenda , ananipikia, hufua nguo zangi ka mikono yake mwenyewe na sio mashine, amnaniheshimu na anatambua nafasi yangu kama mwanamume, pia anatambua nafsi yake kama mwanamke
chanzo: bbc

Comments