Ukungu (fangasi) - ambao umeboreshwa kisayansi kutoa sumu ya buibui - unaweza kuua idadi kubwa ya mbu wanaoambukiza malaraia, utafiti mpya wa kisayansi umebaini.
Majaribio ya ukungu huo, ambayo yamefanyika nchini Burkina Faso, Afrika Magharibi yameonesha kuwa idadi ya mbu iliteketezwa kwa 99% ndani ya siku 45.
Watafiti wanasema si lengo lao kutokomeza mbu hao bali kusaidia kuzuia maambukizi ya malaria.
Ugonjwa wa malaria, unaoambukizwa na mbu jike aina ya Anopheles wanyonyao damu huua zaidi ya watu 400,000 kwa mwaka.
Duniani kote, wagonjwa milioni 219 wa malaria kila mwaka huripotiwa.
Wataalamu hao kwanza walianza kwa kutambua kuvu ama ukungu aina ya Metarhizium pingshaense ambao kiasili kudhuru mbu waambukizao malaria.
Hatua iliyofuatia ilikuwa ni kuuongezea nguvu ukungu huo.
"Kuvu hiyo ni rahisi kuiongezea kitu kisayansi, hivyo ni rahisi kuifanyia uhandisi jeni," amesema Profesa Raymond St Leger, kutoka Chuo Kikuu cha Maryland.
chanzo: bbc
Comments
Post a Comment