Aidha uongozi wa Yanga umeshauri kuanzisha utaratibu wa kuhuisha mikataba ya wachezaji kabla haijamalizika ili kuondokana na 'presha' ya usajili mwishoni mwa msimu
Hawa hapa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika Yanga;
Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani (alitolewa kwa mkopo), Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma, Matheo Anthony na Mrisho Ngasa
wengine ni Thabani Kamusoko, Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Pius Buswita, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali, Ibrahim Ajib (anaenda TP Mazembe), Amissi Tambwe na Haruna Moshi
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kabla hajasafiri kwenda Congo kujiunga na timu ya Taifa wiki ijayo, timu hiyo itakamilisha usajili wa wachezaji wapya nane
Bila shaka pia itakuwa imemalizana na wachezaji waliopendekezwa kuendelea kubaki Jangwani
Comments
Post a Comment