Maajabu hutokea ambapo watu wengi wanakuwa hawatarajii. Liverpool waliingia uwanjani wakichukuliwa kama wanyonge AKA 'underdogs. Hata wachezaji wa Barca na wenyewe walikuwa kama vile wamekuja Anfield kukamilisha ratiba tuu. Amini usiamini' Liver waliuanza mchezo kwa kasi isikuwa ikitarajiwa. Wengi tulijua ni nguvu ya soda tu ambayo hufifia dakika chache baada ya chupa kufunguliwa. Taratibu, mawazo ya watu yalianza kubadilika dakika ya 7 tu ya mchezo pale Divock Origi alipousukumizia mpira wavuni baada ya kipa wa Barca ter Stegen kuutema mpira kufuatia shuti la nahodha wa Liverpool Jordan Henderson. Liverpool waliendelea na sakasaka hadi kipindi cha kwanja kikamalizika. Katika kipindi cha pili timu zote mbili zilifanya mabadiliko kadhaa, lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kwa upande wa Liverpool kuingizwa kwa Mholanzi Georginio Wijnaldum ambaye aliwanyanyua wazee wa 'You will never walk alone' kwenye viti vyao dakika ya 54 na dakika mbili baadae akaigongelea Barca msumari wa kichwa kwa kupachika bao zuri la kichwa. Akina Messi walijaribu kufanya yao lakini wapi! katika dakika ya 79 D. Origi alirudi tena nyavuni na kuwahitimishia hesabu na furaha majogoo wa London kwa kufunga bao rahisi kutokana na kona iliyochongwa kiufundi na Alexander Arnold. Hadi mwisho wa mchezo Liverpool 4 na Barcelona 0.
7'
1 - 0
11'
45'
53'
54'
56'
66'
75'
79'
Comments
Post a Comment