Baba yangu aliwahi kuniambia ,Usije thubutu kumuacha mkeo kwa sababu zako binafsi , ukaoa mke mwingine, na usije thubutu Kumuongezea Mkeo ,Mke wa pili.
Kiukweli wakuu, kama mtatoa muda wa kutafakari sanaaaa Baadhi ya Vifo vya wanaume wengi hapa Dunian hususan Tanzania Yetu,, Vifo vingi sana vya wanaume walofanikiwa kimaisha kisha wakaamua kumuacha mke waliyesota naye kutafuta maisha na kuoa mwanamke mwingine, au Kuongeza mke wapili.....
Basi Siku Mwanaume huyu akifa, Kama sio Kifo cha haki ,basi kuna Uwezekano mkubwa wa Mke wa Pili kuhusika na kifo hicho... Kwann mke wapili?? Kwa sababu anakua hana uchungu na wewe, mara nyingi wanaolewa kwa sababu hasa hasa za Kimaisha yaani hakupendi isipokuwa hamna namna , kiukweli kabisa, Ukiachana na masuala ya kidini ,HAMNA MWANAMKE ANAYEPENDA KUWA MKE WA PILI ,KILA MWANAMKE ANATAMANI AMMILIKI MUMEWE YEYE MWENYEWE KWA KUWA WAMEUMBWA NA MOYO ILIOJAA WIVU .
Ukikuta Anatamani kuwa mke wa pili ,basi anakuwa kuna kitu kilichombana kiasi kwamba anaona "Nipo tayari "kubadili" dini, nipo tayari kuwa "hata" mkeo wa pili"....( na huyu ukishindwa kumuoa, Utasikia anasema "Nizalishe basi niwe na mtoto wako"".
Tena bora ya hawa ambao toka wanazaliwa Dini inawafunza kuwa mke wa pili, au watatu au wanne ... lakini hawa wengine ukishamuoa au kumfanya mchepuko, Atataka sasa aingilie mpaka ya ndani au mpaka mgombane na mkeo mkubwa n.k n.k
hebu fanyeni utafit , angalieni vifo vyenye ukakasi ,ukakasi huo ulitokana na nani??
,MKE WA PILI NI SAWA NA SIMBA AWINDAE KIMYA KIMYA .
Mtizamo tu!!
By Carlos The Jackal/JF
edited by William Chazega
Comments
Post a Comment