Fursa ya kufundisha Kiswahili Afrika Kusini, wasomi mpo?

Image result for swahili language
Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wameafikiana kuhusu kufundisha lugha yaKiswahili, ikiwa ni siku chache toka mawaziri wa Kenya na Afrika Kusini kusaini makaubaliano kuhusu suala hilo.
Rais Magufuli alikutana na Ramaphosa Ikulu ya Pretoria Jumapili, Mei 27 2019, ikiwa ni siku moja tu toka Ramaphosa alipoapishwa kuendelea kuliongoza taifa la Afrika Kusini.
Katika mkutano huo faragha, Magufuli alimpatia zawadi ya vitabu vya Kiswahili mwenyeji wake pamoja na kamusi.
Afrika Kusini iliidhinisha lugha ya Kiswahili kufundishwa katika shule za nchi hiyo Septemba 2018 kuanzia mwaka 2020 na kufungua fursa kwa walimu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki amapo lugha hiyo ndipo inapochimbukia na kuzungumzwa.
Taarifa rasmi ya Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bw Gerson Msigwa inasema kuwa: "Rais Ramaphosa amesema kufuatia uamuzi wa Afirka Kusini kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo katika shule za msingi na sekondari."
Katika video fupi ambayo imepakiwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter wa Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbas, Rais Magufuli anasema kuwa makubaliano hayo pamoja na ya ushirikiano katika nyanja nyengine kama uchumi tatatiwa saini katika ziara rasmi ya Ramaphosa nchini Tanzania kabla ya kufanyika kwa mkutano wa ukanda wa SADC mwezi Agosti mwaka huu.
Wakati Marais hao wakifikiana makubaliano hayo, tayari Mawaziri wa Elimu wa Kenya Profesa George Magoha na Afrika Kusini Angelina Matsie Motshekga wametiliana saini makubaliano ya Kenya kupeleka walimu wa somo hilo.
Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Nairobi Mei 16.
source:bbc

Comments