Baba 'amuuza' mtoto kwa wauaji Tanzania kwa $2,000

Ulrich Matei nchini Tanzania inawashikilia watu wawili kwa mauaji ya mtoto wa miaka sita ambayo yanahusianishwa na imani za kishirikina.
Washukiwa katika kesi hiyo ni baba wa mtoto na mmiliki wa shule moja ya sekondari katika mkoa wa Mbeya, nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Kamanda wa Polisi wa Mbeya Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku 10 zilizopita (Mei 03), ambapo baba anadaiwa kumuuza mtoto wake kwa wauaji kwa Sh5 milioni takribani $2,200.
"...(baba) alikubali kumtoa mtoto wake kwa (jina linahifadhiwa) ambaye ni mfanyabiashara wa shule ya sekondari ili ili akatwe kanyagio la mguu wa kulia kwa ajili ya kutengenezea ndagu (dawa ya utajiri) kwa ajili ya kuendeshea biashara zake," Kamanda Matei amewaambia wanahabari.
Polisi wanabainisha kuwa mwili wa mtoto huyo ulitupwa katika msitu wa Hifadhi wa Chimala wilayani Mbarali na baada ya baba wa mtoto kukamatwa alikiri kuhusika na kueleza kuwa mguu wa mtoto umefukiwa kilomita 70 kutoka eneo alipouawa wilayani Mbalizi.
"Baada ya mmiliki wa shule kutajwa na kukamatwa, alikiri kuhusika na tukio hilo na wawili hao wapo mahabusu kupisha uchunguzi zaidi,"amesema Kamanda Matei.
Kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi ikiwemo kumsaka mganga aliyehusika na tukio hilo. 
source: bbcswahili

Comments