AJIBU AKWAMA MAZEMBE

Klabu ya TP Mazembe imeachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib Migomba, imefahamika


Kulingana na taarifa iliyopatikana mapema leo, TP Mazembe imeushukuru uongozi wa Yanga kwa ushirikiano waliotoa tangu mchakato wa kumuwania kiungo huyo ulipoanza


Hata hivyo Mazembe haijaeleza sababu ya uamuzi wake wa kuachana na Ajib


Suala la maslahi linatajwa kuwa moja ya sababu iliyokwamisha 'dili' hiyo


Aidha vyanzo vingine vinataarifu kuwa klabu ya Simba imeingia kati na iko karibu kumsajili kinara huyo wa kupika mabao msimu huu licha ya uongozi wa Yanga kuwa katika mazungumzo nae ili asaini mkataba mpya


Comments