Mateja Tanzania wageuza dawa ya panya kilaji


Kuadimika kwa mihadarati kama cocaine na heroine Tanzania ni matokeo ya juhudi za serikali ya nchi hiyo kupambana na uingizwaji na usambazaji wa dawa hizo haramu nchini humo.
Waraibu wa dawa za kulevya, ambao wanafahamika kwa jina la mateja nchini Tanzania sasa wanachanganya sumu hiyo ya panya na dawa nyengine haramu za kulevya kama bangi na kisha kuvuta pamoja.
'Upatikanaji wa sumu ya panya ni rahisi sana hasa katika maduka ya bidhaa za nyumbani na kwenye masoko, na huuzwa kwa bei ya chini.
Si rahisi kumtilia shaka mnunuzi wa sumu ya panya, kufanya hivyo si kinyume cha sheria. Ila kwa sasa kinachosalia baada ya manunuzi ni jinsi gani sumu hiyo inaenda kutumika.
Wataalamu wa Afya wameiambia BBC kuwa matumizi ya sumu hiyo kama kilevi ni hatari zaidi ya dawa za kulevya za asili kama Coccaine na Heroine.
Wakati mamlaka nchini humo zikiendelea kupiga hatua dhidi ya wafanyabiashara wakubwa na wakati wa dawa za kulevya, ni dhahiri kuwa bado kuna changamoto kubwa ya kudhibiti watumiaji, ambao kila uchao wanatafuta aina mpya ya dawa kukata kiu ya uraibu wao.
Mwaka jana, BBC pia iliripoti namna waraibu wa mihadarati nchini Tanzania wamegeukia dawa za usingizi kama njia mbadala baada ya kuadimika kwa dawa za kulevya.
chanzo: bbc swahili


Comments